Jamaa kutoka Somalia afanya ndoa ya kipekee na bi harusi 2
- Jamaa huyo aliwaposa wanawake hao wawili kwa wakati mmoja kabla ya kuwaomba wawe wake zake
- Alisema kuwa alitaka kuwaoa wote wawili kwa sababu alitaka kuwa na watoto wengi
Jamaa mmoja raia wa Somalia alijawa na furaha mpwito baada ya kujinyakulia wake wawili kwa wakati mmoja katika harusi iliyofana sana.
Jamaa huyo, Bashir Mohamed na mabinti hao wawili waliofahamika kama Iqra na Nimo waliandaa harusi ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na mamia ya washiriki.
Habari Nyingine: Mwanamume amnunulia Samantha wake gari la KSh 2 milioni
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC, Mohamed aliwachumbia wawili hao kwa muda wa takriban miezi minane kabla ya kuwaomba wawe wake zake.

Habari Nyingine: Wazir Chacha, mwanamume aliyedaiwa kushiriki ngono na wabunge, arejea kwa mpigo
Alisema kuwa kupitia kwa harusi hiyo yake, wanaume wengi watakuwa na moyo wa kufuata mwelekeo aliochukua.
"Nilikuwa nawaambia peupe wote wawili kuwa nawapenda. Waliridhika," Alisema.
Habari Nyingine: Picha za watoto wa mtaani wakifanya harusi Gikomba zafurahisha wengi
Kulingana na Mohamed, nia yake ya kuwaoa wawili hao ni kupata watoto wengi.
Pia, aliamua kufanya harusi ya pamoja ili kuboresha uhusiano kati yao.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIVxf49moZqlkZZ6rMHTqKKaZaOkuqK4yJpkmp6Ro8aiec2dppplqZZ6rLXPnqKenV2jrm6uyGafmqqlqLZufo2hq6ak